Jumanne 8 Julai 2025 - 21:57
Raisi wa Muungano wa Umoja wa India: Imam Khamenei si kiongozi wa Iran pekee, bali ni kiongozi wa Waislamu wote duniani

Hawza/ Salman Nadwi amesema: Imam Khamenei si Kiongozi Mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pekee, bali ulimwengu mzima wa Kiislamu na mataifa yote ya Kiislamu yameamua kwamba yeye ni kiongozi wa Waislamu wote na mataifa yote ya Kiislamu.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza Sayyid Salman Nadwi, mwanazuoni wa Kisunni kutoka India na kiongozi wa Muungano wa Umoja (Jabhat al-Ittihad), katika kikao cha nne cha mtandaoni cha "Ummah Moja" kilichoandaliwa na Jabhat Izzat al-Islamiyya, alisema kuwa:

Natoa pongezi kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kwa Imam na Kiongozi Mkuu Sayyid Ali Khamenei al-Huseini, na kwa taifa lote la Iran. Taifa la Iran, uongozi wa Iran, na Kiongozi Mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu wamethibitisha kuwa wao ni waongozaji na waasisi wa harakati ya Imam Mahdi (af) na wako katika njia sahihi, na wanapambana kwa uthabiti na adui mkubwa wa haki "Dajjal" pamoja na watangulizi wake ambao ni Wazayuni, Wakristo wa Kizayuni, Wamarekani, na Wazayuni wa Kiarabu walio fisadi. Msimamo huu wa kusimama imara unapaswa kuwa wa kudumu daima.

Aidha, hivi sasa ulimwengu mzima wa Kiislamu umesimama nyuma ya Imam Khamenei. Imam Khamenei si kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pekee, bali mataifa yote ya Kiislamu na ulimwengu wote wa Kiislamu wamekubali kwamba yeye ni kiongozi wa Waislamu wote na wa mataifa yote ya Kiislamu. Tunampongeza kwa hilo.

Ni matumaini yetu kwamba, Imam Khamenei ataendelea na mapambano haya makali na ya kuamua hatima hadi tufikie kwenye tukio kubwa la kihistoria ambalo Mtume (saww) alilitaja – tukio ambalo litaonyesha wazi kwa watu wote kwamba Mahdi (as) ndiye atakayelivisha ushindi suala la Palestina na kuleta ushindi juu ya ulimwengu mzima – na hakika waongozaji wa harakati hiyo wapo, na wao ndio wanaoliandalia uwanja wa kudhihiri kwa Imam Mahdi (as).

Majma‘ Al-'Alamī Qādimūn.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha